JE UNAO UZIMA WA MILELE?
Swali: "Je, unao uzima wa milele?"
Jibu: Bibilia inaonyesha njia ya wazi ya uzimani. Kwanza, ni sharti tutambue yakwamba tumetenda dhambi kinyume chake Mungu: “Kwasababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 3:23, TMP). Sote tumefanya mambo ambayo hayampendezi Mungu, ambayo yanafanya tustahili adhabu. Na kwakuwa dhambi zetu tuzitendazo mwishowe ni dhambi zinazomlenga Mungu wa umilele, basi ni adhabu ya milele pekee tunayostahili kuadhibiwa. “Kwa maana mshahara wa dhambi ni kifo; lakini zawadi anayotoa Mungu ni uhai wa milele katika kuungana na Kristo Yesu, Bwana wetu” (Warumi 6:23, BHN).
Hata hivyo Yesu Kristo, milele Mwana wa Mungu asiyekuwa na dhambi (1 Petro 2:22), alifanyika kuwa mwanadamu (Yohana 1:1,14) na akafa ili kutulipia adhabu yetu. “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi” (Warumi 5:8, TMP). Yesu Kristo alikufa msalabani (Yohana 19:31-42), achukue adhabu ambayo sisi tulistahili (2 Wakorintho 5:21). Siku tatu baadaye akafufuka katika wafu (1 Wakorintho 15:1-4), kudhihirisha ushindi Wake juu ya dhambi na mauti. “kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu” (1 Petro 1:3, TMP).
Kwa imani, ni sharti tuwe na badiliko la akili kuhusu Kristo - yaani Yeye ni nani?, kile Alichokifanya?, na kwanini alikifanya? - kwasabu ya wokovu (Matendo 3:19). Kama tukiweka imani yetu Kwake, kwa kuamini kifo chake pale msalabani kama malipo ya dhambi zetu, tutasamehewa na kupokea ahadi ya uzima wa milele kule mbinguni. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16, TMP). “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka” (Warumi 10:9, TMP). Imani pekee katika kazi aliyo ikamilisha Kristo pale msalabani ndiyo njia ya kweli na pekee ifikayo uzimani! “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, wala si kwa matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu, si kwa matendo, ili mtu awaye yote asije akajisifu.” (Waefeso 2:8-9, KCV).
Ukiwa unataka kumpokea Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako, tazama mfano huu wa maombi. Kumbuka ya kwamba, kusema ombi hili au ombi lingine lolote lile halitakuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo peke yake ndiko kutakuokoa toka dhambini. Ombi hili ni njia nyepesi ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu, najua yakwamba nimetenda dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo ameichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Naweka imani yangu Kwako pekee ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako ya ajabu, na msamaha - zawadi ya uzima wa milele! Amina!”
No comments