MUME AU MKE SAHIHI
NJIA TATU ZA KUJUA MUME/MKE WAKO SAHIHI.
Shalom Aleikem wana Mungu ni wakati mwema sana katika kutafakari maarifa haya ya neno la Mungu karibu katika ujumbe huu na Roho mtakatifu akupe kuyajua haya katika Jina la Yesu.
Moja kati ya jambo ambalo limekuwa ni gumu kwa vijana walio wengi ni kujua mke/mume sahihi wa kuishi naye katika Ndoa.Na vijana wengi wameingia ndoa nyingi kimakosa nyingine zimevunjika mda mchache,ila zipo ambazo zimejaa karaha na mateso.Kijana ambae ujaoa/kuolewa ni vyema ukafuatilia somo hili ili uwe na maarifa ya kukusaidia juu ya safari yako.
Hatuna budi kufahamu ili upate kitu chema kutoka kwa Mungu ni lazima nawe uishi vile Mungu anataka yani uishi katika UTAKATIFU,si uishi katika UTAKATIFUƁkwa lengo la kupata mke/mume lahasha bali lazima utambue pasipo UTAKATIFU hakuna atakayemwona MUNGU.
15 bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;
1 Petro 1:15
1 Petro 1:15
Tunaona maandiko yanasisitizia 👆👆👆 Tuwe watakatifu katika mwenendo wetu wote,hii ina maana ya kwamba tukiwa watakatifu tunao ujasiri wa kwenda Mbele za Baba yetu wa mbinguni na kumuomba kile tunachohitaji,kwa sababu Mungu anawasikia watakatifu tu,hivyo basi kabla ujaomba uyo mke/mume mwema huna budi kujioji wewe ni mwema/mtakatifu?.Kama jibu ni la ni vema ukatengeneza Mungu wako na kama ujaokoka ni vema ukaokoka kwa ajili ya kwenda mbinguni na si kwa ajili ya mme/mke tu.
Njia hizi zitakusaidia kutambua mume/mke sahihi wa maisha yako.
1.. AMANI YA KRISTO.
Hii ni Amani ya Bwana Yesu kristo ndani yako na Amani hii huja ikiwa ndani yako umeshiba neno la Mungu. Amani hii ikiwepo ndani yako kama mwanaume/mwanamke huyo si sahihi utaona ndani yako unakosa Amani juu yake,pengine mtu yule si mzuri kuishi naye ndani ya ndoa,pengine ni wakala wa shetani,labda anaigiza wokovu ili akunase utaona kabisa ndani yako unakosa Amani juu yake,ukiona hivyo ni vyema kusitisha mahusiano hayo kwa Maana ni Mungu anakutadharisha juu hilo.
Ila unapoona Amani juu ya mwanaume/mwanamke huyo basi jua upo sehemu sahihi,atakuwa ameokoka,anaishi maisha matakatifu,moja kwa moja Amani ya kristo itakuongoza juu ya mtu huyo na mtakuwa huru kuishi naye katika ndoa.
Ila hatuna budi kufahamu kuna Amani za kibinadamu na si Amani ya kristo Yesu,unamkuta dada anakosa Amani na mwanaume huyo sababu hana gari,nyumba ,pesa nk,hii siyo Amani ya kiMungu.
15 Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.
Wakolosai 3:15
Wakolosai 3:15
Rejea maandiko👆👆👆 kuwa na Amani ya KiMungu ndani yako juu mwanaume/mwanamke huyo ni ishara ya wazi kabisa ni mtu sahihi kwako,usingoje ndoto au maono juu ya mme/mke wako vilevile lazima ujue pia Amani ya Kristo inatuongoza pia kufanya maamuzi sahihi juu ya kupata mme/mke sahihi.
2...UFUNUO.
Ufunuo ni kitu kilicho fichwa na kuwekwa wazi.hapa hatuna budi kuwa makini sana,ufunuo waweza kuwa ndoto au maono,lazima ujue kuna ndoto au maono ya Mungu ,na kuna ndoto au maono ya shetani,vile kuna ndoto za kumuwaza mtu sana matokeo yaku unamuota.
Tunachoangalia hapa ni ni ndoto au maono ya Mungu ,hatuna budi kufahamu Mungu anaweza kukuonyesha Mke/mume wako ndoto au maono ila ni lazima ujue kupambanua sana ,maana shetani pia anaweza kutumia njia iyo akakuonyesha wake matokeo yake ukapotea.
Kwa kuwa sikuipokea kwa mwanadamu wala sikufundishwa na mwanadamu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo.
Wagalatia 1:12
Rejea andiko hilo Paulo mtume anaweka wazi kuwa elimu ya Mungu hakuipokea kwa mwanadamu bali kwa ufunuo wa kristo,Tunajifunza nini kumbe ufunuo unatoka sehemu mbalimbali,hivyo ni vyema kuthibitisha je uyo mke/mume ni kweli umeonyeshwa na Mungu? Je utajuaje jibu ni rahisi,Lazima awe amebeba sifa za KiMungu ndani yake yani UTAKATIFU nk.
3....KUPENDA.
Ni njia moja wapo ambayo pia inaweza kukuhalalishia kuwa uyo ni mme/mke wako sahihi,hapo ni upendo wa KiMungu kaka usimpende binti kwa sababu anaumbo na namba nane,sina maana ya kwamba usivutiwe naye lahasha yani upendo wako usiwe juu kitu fulani ndani yake,au dada usimpende kijana kwa sababu ya cheo,au mali ukasema huyu anafaa kuwa mme wangu ,ikitokeo mali zimepukutika na upendo unaisha.
Upendo unaongelewa hapa ni ule upendo wa KiMungu juu ya uyo mke/mume wako ambao moyo wako unasema iwe raha,iwe shida ,iwe njaa,iwe kulala chini nipo tayari huo ndo upendo.
6 Bwana ameagiza neno hili katika habari ya binti za Selofehadi, akasema, Na waolewe na waume wawapendao; lakini na waolewe katika jamaa ya kabila ya baba zao.
Hesabu-Numbers 36:6
Hesabu-Numbers 36:6
Angalia mstari huo 👆👆 biblia inasema WAOLEWE na WAUME WANAO WAPENDA,kwaiyo usisubiri ndoto au kuonyeshwa unapoona unaupendo na mwanaume/mwanamke huyo ni kiashiria kuwa ni mtu huyo ni sahihi,ila lazima awe ametimiza vigezo vya KiMungu ndani yake ,ameokoka,naishi maisha ya utakatifu,nk
Asante sana kwa ushauri,maombi,au kujiunga na group letu la watsup basi nitafute kwa namba hapo chini.
0755722778 sms au piga
0755722778 watsup
0755722778 watsup
No comments