Nguvu ya Kusamehe na kusahau

Sameheni saba mara sabini. Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao na Baba yenu wa mbinguni atawasamahe ninyi, (Mathayo 6: 9ff). Watu wengi katika Kanisa la leo wana tatizo ndani yao: Tatizo la kutosamehe. Wapo watu ambao wanasali, wanatoa sadaka, n.k., lakini hawataki kusamehe ati mpaka wakapatane mbinguni. Neno hili lina nguvu kwa sababu Mungu aliutoa uhai kwa makosa yetu, nasi tumesamehewa. Tatizo tulilonalo sisi tuliosamehewa kwa thamani ya kifo (damu na uhai) wa mwana wa Mungu, ni kutosamehe. Una kipaji cha uimbaji au lolote lile – bila kusamehe sahau mbingu. Watu ambao hawajasameheana hawaingii mbinguni. Unajua watoto wanapatana hata kama wazazi wao wa pande mbili wana ugomvi. Sisi tunawakoroga na kuwaingiza kwenye ugomvi wetu. Bila kusahau hakuna amani. Wengi hawawezi kukaa pamoja, kisa wana ugomvi. Wengine wananena kwa lugha na kwa ufundi sana katika maombi lakini hawajasameheana na wenzao. Hivi ni nani anakudanganya kuwa hayo ni tiketi ya mbinguni? Yesu alichuruzika damu na kutoa uhai lakini akasema: “Usiwahesabie dhambi hii.” Stefano hali kadhalika alisema: “hawajui walitendalo uwasamehe.” Tusiwe na ulokole wa unafiki. Mlokole mnafiki asili yake: Balokole yaani ‘watu wasio na mbele wala nyuma.’ Watumishi wanawaombea watu wanapita lakini waombaji hawapiti. Hawasalimiani, hivyo hawapiti wakati mwingine wanajiosha mbele za watu lakini ndani ni tatizo kubwa sana. Watu kusameheana na kuachiliana ni lazima. Hakuna mahusiano ya mtu na Mungu bila msamaha: Marko 11:25, “Nanyi kila msimamapo kusali sameheni.” Kinyume cha hapo Mungu hatasamehe. Ukisimama po pote kusali hakikisha huna mtu uliyemfunga moyoni mwako. Wengine wanasimama kanisani, kwenye jumuiya au nyumbani kusali lakini sala hiyo haiendi kwa Mungu kwa sababu ndani yake amebeba chuki badala ya Yesu. Hivyo hawaoni neema ya Mungu mpaka hapo atakapo achilia watu aliowafunga ndani yake. Nguvu mbaya ndani ya moyo ya kifungo cha chuki inasimamiwa na shetani. Baba, Mwana na Roho Mtakatifu hawata kusamehe wewe usiposamehe wale unaokaa na kuhusiana nao. Sharti wasamehe kwanza ndipo wewe usamehewe. Yoh 9:3 tunasoma: “Mungu hawasikii wenye dhambi.” Chuki ni sehemu ya dhambi. Unapotembea na watu moyoni na huwaachilii ni dhambi. Heri ufanye haraka kabla Yesu hajawahukumu. Unapomshusha mtu au kumtukana mtu kwa siri ni dhambi. Watu wanaweka ukuta kwa ajili ya wenzao. Huwezi kuondoa kibanzi ndani ya jicho la mtu wakati wewe una boriti. Toa boriti lako kwanza halafu kibanzi chake. Huwezi kumpenda Mungu wakati hujampendeza unaemwona. Huwezi kumpenda Mungu na jirani yako humpendi. Kumchukia mtu ni kujibebea dhambi. Nguvu ya kusamehe na kuachilia Kusamehe ni lango, na kutosamehe ni lango. Musa alikuwa na wana wa Israel walikuwa wanamwona Mungu wazi wazi. Kwenye matendo makuu baharini. Walipokengeuka na kutengeneza ndama, Mungu akachukizwa kwa kukosewa. Lakini Musa akasogea mbele za Mungu kuomba msamaha. Na Mungu alisamehe. Hakuona namna ya kuendelea kutosamehe. Yesu Kristo alipoteswa alisamehe yote. Hakuna jinsi. Kusamehe, kuachilia na kusahau ni lango la kuingilia katika ndoa, biashara au hali ngumu ya maisha yako. Mtu ambaye hayuko tayari kusamehe, kuachilia na kusahau ni lango la mapepo. Ukiwa umemchukia mtu mapepo yanaingia kirahisi. Mume umemweka moyoni, mfanyakazi na wengine wengi. Mungu akishuka anaona moyo wako ni jalala, mahali pa kutupia uchafu, (maganda ya ndizi, mabaki ya chakula, matakataka). Hapo ndipo Mungu anakosa mahali pa kuingia. Linda moyo wako usiwaweke watu wanaokwaza. Kutosamehe ni lango la magonjwa kuingia (pressure, kisukari, n.k) Utakufa kabisa usipo wasamehe, achilia na kusahau. Utawaweka wangapi moyoni? Raha jipe mwenyewe. Wasamehe bure adui na watesi wako. Mioyo yetu inatakiwa iwe na amani, isiwe na mashaka, iwe na furaha. Utawaweka wangapi katika moyo? Matukio ni mengi duniani. Wanaotuudhi ni wengi sana. Mkaribishe Yesu kwa usalama wa moyo wako. Wanaokasirika na kufanikiwa kwako ni wengi sana. Mioyo inawakera. Hao ni wengi kuliko watu wema. Utawaweka wapi? Jifunze kufungua milango ya kusamehe kuachilia na kusahau.

No comments