JEHANAMU INATISHA

Mwinjilisti PROCESIUS PROSPER

 
WALIOPO JEHANAMU YA MOTO LEO HAWAFAI KUANGALIA WANATISHA.

Shalom wana Mungu ni wakati mwingine katika kutafakari maarifa haya tupate kuwa na moyo wa toba juu ya maisha Yetu ya kila siku.

Jehanamu ya moto ni mahali pa mateso mazito yasiyoeleza na Mungu alipaweka mahususi kwa ajili ya shetani/ibilisi pamoja na malaika zake ambao walifanya uasi kule mbinguni.

Mtu wa Mungu huna budi kufahamu Jehanamu ya moto ni mahali pabaya penye mateso ya mauti ila ufi,Biblia inasema mshahara wa dhambi ni mauti,hii ina maana ni kutupwa Jehanamu ambamo kule watu wanapa mateso yaliyo jaa kufakufa ila hawafi.

Najaribu kukueleza huone ubaya wa mahali hapo,ili usifurahie kuishi maisha ya dhambi ukaona kuwa umefika nataka ujue ipo ghadhabu ya Mungu kwa wale wote ambao wanakwenda kinyume na mapenzi ya Mungu wakiwa hai leo.

Jehanamu ya moto ni moto usio zimika ni moto wamilele sio moto tu wamo funza ambao wao ni maalum kwa ajili ya kuwatesa wale waliomo ndani ya moto huo,kazi ya hawa funzi ni kuwatoboa watu waliomo ndani ya moto huo,cha kushangaza funza hawa hawafi ndani ya moto huo.

Mtu wa Mungu ebu piga picha moto ni mkali na moto huo hauzimi kibaya zaidi wamo funza piga picha unateseka hivyo milele 😃 ooooh inatisha kama nini mtu wa Mungu ,huo ndo ubaya wa dhambi.

Kutokana na mateso haya mabaya na mazito imepelekea watu hawa kuharibika hata kutofaa kutazamika ila wapo hai,utasema ulikufa ukaenda huko ukaona oooh mtu wa Mungu maandiko matakatifu yanathibitisha hilo 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

24 Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.
Isaya 66:24

Angalia maandiko hayo 👆👆👆👆 yana sema" NAO WATATOKA NJE "watakao toka Nje ni watakatifu waliopo mbingu kuja kutazama hawa wanapata mateso katika yenye MOTO USIO ZIMIKA NA FUNZA kama maanɗiko ya semavyo maandiko yana zidi kusema "WATAKUWA CHUKIZO PA WOTE WENYE MWILI" Yani hawafai kutazamika kutokana na mateso yale,oooh Mungu atusaidie sana tusifike huko😃.

Ndugu yangu unajijua unaishi maisha ya dhambi leo amua kufanya toba kweli ,Jehanamu ni pabaya kuliko unavyodhani,tumepewa nafasi moja tu na baada kufa ni hukumu #WAEBRANIA 9:27 ,Unaishi maisha machafu yasirini huku umetangaza umeokoka nataka nikwambie siku ile utawekwa wazi na utakuwa umesha chelewa.

Asante sana mwenye masikio na Asikie Bwana aliambia kanisa kwa ushauri,maombi ,kuokoka au kujiunga na group letu karibu.

0755722778watsup tu

No comments