JIADHARINI NA TAMAA YA MIILI

        
Mwinjisti procesius prosper







WAASHERATI NA WAZINZI SEHEMU YAO NI JEHANAMU YA MOTO.
Shalom wana Mungu ni wakati mwingine tena tukizidi kujifunza maarifa haya ya neno la Mungu tuzidi kuwa safi mbele za Mungu.
Hatuna budi kufahamu maana ya maneno haya kabla kwenda katika ujumbe wetu,UASHERATI NA UZINZI.
UASHERATI Ni kitendo cha kijana wa kiume/kike ambaye hajaoa/kuolewa kujihusisha na ngono
UZINZI ni kitendo ambacho hufanywa na wanandoa mmoja au wote kutoka nje ya ndoa yao na kufanya ngono na mwanaume/mwanamke mwingine mbali na mke/mume wake.
Mpaka hapo umepata maana za maneno hayo ,moja kati dhambi ambazo zinaharibu na kuondoa utukufu wa Mungu juu ya mtu ni zinaa,sina maana ya kwamba dhambi nyingine haziondoi utukufu wa Mungu lahasha,ndo maana maandiko matakatifu yanatutaka tuikimbie zinaa kwa maana ni dhambi pekee ambayo inafanyika juu ya mwili na kumbuka mwili ni hekalu la Roho wa Mungu.
Mtu wa Mungu Yusuph alifahamu hilo ndo maana alikimbia zinaa pale mke wa potifa alipotaka kulala naye ila Yusuph akamjibu "NIMTENDEJE MUNGU UBAYA MKUBWA NAMNA HII" utaona jinsi gani Yusuph alichukulia zinaa ni dhambi ambayo ina muhuzunisha Mungu kupita kawaida ni dhambi ambayo hata toba yake ni gharama kubwa kwa kuwa hufanyika kwa makusudi/kupangwa.
Hatuna budi kufaham mshahara wa dhambi ni mauti na mauti yenyewe ni kwenda Jehanamu ya moto milele,leo unafurahia kufanya uchafu wako pasipo kujiuliza nini hatma yake baada hilo,unafanya bila hofu yoyote kana kwamba Mungu hayupo.
Mume/mke unamuacha mke/mume wako unaenda kwa makahaba huko na kutoa kashfa kwa uyo kahaba wako na kusema ooh mke/mume wangu hanivutii kabisa na kumpa sifa nyingi uyo kahaba wako,nakumuona uyo kahaba ni bora kuliko mme/mke wako wa ndoa,nataka ni kwambie usipotubu na kumuomba mke/mume wako msamaha Jehanamu ya moto inakusubiri milele.
Kijana unajiona wewe ni kidume cha mbegu na kulala na binti ovyo na wake za watu tena unajisifu kabisa nakusema hakuna mwanamke wa kukusumbua akili nataka nikwambia nafasi ya kutubu unayo sasa kabla mlango haujafungwa.
Binti kwa sababu ya uzuri wa sura yako umekuwa ukijiweka kikahaba,mavazi yako kikahaba yani ya nusu uchi unatumia mtego huo kuwanasa vijana na waume za watu umelala na wanaume kibao,unafika mbali unajisifu kwa ukahaba wako nataka ni kwambie utavuna unachopanda,salama yako ni kutubu leo na kuja kwa Yesu kristo.
Yawezekana umekutana ujumbe huu ila Jana umetoka kufanya zinaa,mtu wa Mungu Bwana anakutaka utubu kabla ujaipoteza nafsi yako ,tambua moja dhambi ni tamu ila mwisho wake ni mbaya kuliko unavyo dhani.
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; #waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala #wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,
1 Wakorintho 6:9
Rejea maandiko hayo 👆👆👆 hakuna nafasi ya waasherati na wazinzi katika ufalme wa Mungu,bali sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti,oooh! Inatisha kama nini mtu wa Mungu,tubu leo nafasi unayo bado ujachelewa ndo maana ujumbe huu umekuja kwa ajili yako.
Asante sana kwa ushauri,maombi,au kujiunga na group letu basi nitafute kwa namba hapo chini.
0755722778
sms au kupiga
0755722778watsup 

No comments