KUVUKA BAHARI NYEKUNDU
Bwana Yesu apewe sifa wana wa mungu ninaamini ya kuwa Mungu wetu mwaminifu amewapa afya njema tena kutokana na hilo ebu tumpe Mungu wetu utukufu na heshima na tuziimbe sifa zake milele amina yeye ni Bwana hakika ni Mfalme wa wafalme ni Mungu wa miungu mbinguni na duniani hakuna kama yeye.Mpendwa ni wakati upi mgumu unapitia wewe ama ni jambo gani linakuzuia usiendelee mbele na safari yako uloianza usirudi nyuma usikate tamaa usinungunike usilie bali tazame YEHOVA yeye atakupa njia yupo mtu mwenye fimbo ya kuyasambalatisha hayo maji yalokuzuia usiione njia wekw tumaini lako kwa MUNGU.
neno la mungu linasema hivi;kut14;1-26
neno la mungu linasema hivi;kut14;1-26
1BWANA akasema na Musa, akamwambia, 2Hes 33:7; Yer 44:1 Waambie wana wa Israeli, kwamba warudi na kupiga kambi yao mbele ya Pi-hahirothi, kati ya Migdoli na bahari, kukabili Baal-sefoni; mtapanga mbele yake karibu na bahari. 3Zab 35:21; 71:11 Naye Farao atasema katika habari za wana wa Israeli, Wametatanishwa katika nchi, lile jangwa limewazuia wasitoke. 4Yak 1:13-17; Kut 9:16; Rum 9:17-23 Nami nitaufanya uwe mgumu moyo wa Farao, naye atafuata nyuma yao; nami nitajipatia utukufu kwa Farao, na kwa jeshi lake lote; na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA. Basi wakafanya hivyo. 5Mfalme wa Misri aliambiwa ya kuwa wale watu wamekwisha kimbia; na moyo wa Farao, na mioyo ya watumishi wake, iligeuzwa iwe kinyume cha hao watu, nao wakasema, Ni nini jambo hili tulilotenda, kwa kuwaacha Waisraeli waende zao wasitutumikie tena? 6Akaandaa gari lake, akawachukua watu wake pamoja naye; 7tena akatwaa magari mia sita yaliyochaguliwa, na magari yote ya Wamisri, na maofisa wa kijeshi juu ya magari hayo yote. 8Kut 6:1; 13:9; Hes 33:3 Na BWANA akaufanya moyo wake Farao mfalme wa Misri kuwa mgumu, naye akawafuata wana wa Israeli; kwa sababu wana wa Israeli walitoka kwa jeuri.14:8 Katika tafsiri nyingine ni ‘ushupavu au ulinzi wa BWANA’. 9Kut 15:9; Yos 24:6 Wamisri wakafuata nyuma yao, farasi wote na magari yote ya Farao, na askari zake wenye kupanda farasi, na jeshi lake, nao wakawapata wakiwa wamepanga pale karibu na bahari, karibu na Pi-hahirothi, kukabili Baal-sefoni. 10Yos 24:7; Neh 9:9; Zab 34:17; 107:6 Hata Farao alipokaribia, wana wa Israeli walipoangalia nyuma na kuona Wamisri wanakuja nyuma yao; wakaogopa sana; wana wa Israeli wakamlilia BWANA. 11Zab 106:7 Wakamwambia Musa, Je! Kwa sababu hapakuwa na makaburi katika Misri umetutoa huko ili tufe jangwani? Mbona umetutendea haya, kututoa katika nchi ya Misri? 12Kut 6:9 Neno hili silo tulilokuambia huko Misri, tukisema, Tuache tuwatumikie Wamisri? Maana ni afadhali kuwatumikia Wamisri kuliko kufa jangwani. 132 Nya 20:15,17; Isa 41:10-14 Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.14Kum 20:4; Yos 10:14; 23:3; 2 Nya 20:29; Neh 4:20; Isa 30:15; 31:4 BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.
15BWANA akamwambia Musa, Mbona unanililia mimi? Waambie wana wa Israeli waendelee mbele. 16Kut 7:19 Nawe inua fimbo yako, ukanyoshe mkono wako juu ya bahari, na kuigawanya; nao wana wa Israeli watapita kati ya bahari katika nchi kavu. 17Mit 29:1 Nami, tazama, nitaifanya mioyo ya Wamisri kuwa migumu, nao wataingia na kuwafuatia, nami nitajipatia utukufu kwa Farao, na kwa jeshi lake lote, kwa magari yake na kwa wapanda farasi wake. 18Na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapokwisha kujipatia utukufu kwa Farao, na magari yake, na farasi wake.
19 Mwa 48:16 Kisha malaika wa Mungu, aliyetangulia mbele ya jeshi la Israeli, akaondoka akaenda nyuma yao; na ile nguzo ya wingu ikaondoka hapo mbele yao, ikasimama nyuma yao; 20Isa 8:14; 2 Kor 4:3 ikawa katikati ya jeshi la Misri na jeshi la Israeli; napo palikuwa na lile wingu na lile giza, lakini lilitoa nuru wakati wa usiku; na hawa hawakuwakaribia hawa usiku kucha. 21Yos 3:16; 4:23; Neh 9:11; Zab 74:13; 106:9 Musa; akanyosha mkono wake juu ya bahari; BWANA akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki, usiku kucha, akaifanya bahari kuwa nchi kavu, maji yakagawanyika. 221 Kor 10:1-2; Ebr 11:29; Kut 15:19; Hes 33:8; Zab 66:6; 78:13 Wana wa Israeli wakaenda ndani wakipita kwenye nchi kavu ndani ya bahari; huku maji yakiwa ukuta kwao mkono wa kulia na mkono wa kushoto. 23Na wale Wamisri wakawafuata, wakaingia ndani kati ya bahari, farasi wote wa Farao, na magari yake, na wapanda farasi wake. 24Ikawa katika zamu ya alfajiri, BWANA akalichungulia jeshi la Wamisri katika ile nguzo ya moto na ya wingu, akalifadhaisha jeshi la Wamisri. 25Akayakwamisha14:25 Katika Kiebrania ni ‘akayaondoa magurudumu’.magurudumu ya magari yao, hata yakaenda kwa shida; na Wamisri wakasema, Na tuwakimbieni Waisraeli; kwa kuwa BWANA anawapigania.
Unapokuwa unavuka ama unatoka kwenye matatizoulokuwa nayo tambua wapo maadui nao wanapambana ili usivuke ama usifanikiwe hawatakata tamaa watafanya kila wawezalo kukurudisha nyuma ila wewe isiangaike nao kwkuwa njia ya mafanikio yako ni kaburi kwa adui yako awezi ipitia njia hiyo akawa salama kut14;26
Wamisri wazama
26BWANA akamwambia Musa, Nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi tena juu ya Wamisri, juu ya magari yao, na juu ya farasi wao. 27Yos 4:18 Musa akaunyosha mkono wake juu ya bahari, na kulipopambazuka, bahari ikarudi kwa nguvu zake; Wamisri wakajaribu kuyakimbia maji na BWANA akawaangamiza hao Wamisri katika bahari. 28Kum 11:4; Zab 78:53; Neh 9:11; Hab 3:8 Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; hakusalia hata mtu mmoja. 29Zab 77:20; 78:52,53 Lakini wana wa Israeli wakaenda katika nchi kavu katikati ya bahari; na hayo maji yalikuwa ni kuta upande wao wa kulia, na upande wao wa kushoto. 30Zab 106:8-10; 58:10; 59:10 Ndivyo BWANA alivyowaokoa Israeli siku ile mikononi mwa Wamisri; Waisraeli wakawaona Wamisri ufuoni mwa bahari, wamekufa. 31Kut 19:9; Yn 2:11; 11:45 Israeli akaiona ile kazi kubwa aliyoifanya BWANA juu ya Wamisri, ndipo hao watu wakamcha BWANA, wakamwamini BWANA, na Musa mtumishi wake.
ubarikiwe na Bwana Ameni
by mwinjilisti prosper
simu 0755722778
No comments